Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema kesho atatembelea ofisi za Clouds Media kwa ajili ya kuwapa pole baada ya ofisi hizo kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na askari.
Gwajima amesema hayo kupitia akaunti yake ya Instagram akieleza hayo kwa lengo la kuwapa pole juu ya tukio la Makonda kuingia ofisi za Media hiyo.
Tukio hilo limeripotiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa RC Makonda alitaka watangazaji wa kipindi cha Shilawadu warushe kipindi ambacho hakijamalizika kwenye maandalizi yake.
Sababu ya mkuu wa mkoa huyo kuvamia ofisi hizo ni kwasababu watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kukataa kurusha habari kuhusu mwanamke aliyezaaa na Gwajima.
Tukio hilo lilitokea siku ya Ijumaa midaa ya saa tano kasoro ambapo mkuu wa mkoa alivamia ofisi hizo akishindikiza kutoka kwa habari yake ambayo ilikuwa na lengo la kumchafua mchungaji Gwajima.