Mshambuliaji wa Ufaransa na klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezman amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu nchini Hispania akiwashinda Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.

Mshambuliaji huyo aliisadia klabu yake kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini humo huku wakifika fainali ya klabu bingwa waliocheza dhidi ya Real Madrid lakini walifungwa kwenye fainali hiyo.

Kwa upande wa kocha bora mshindi ni kocha wa Atletco Madrid, Diego Semioni baada ya kumshinda kocha wa Celta Vigo, Toto Berrizo pamoja na kocha wa Villareal Marcelino.

Tuzo ya beki bora imekwenda kwa Diego Godin wa Atletico Madrid huku kipa bora akiwa Jan Oblak wa Atletico Madrid pia.

Lieonel Messi ameafanikiwa kushinda tuzo ya mshambuliaji bora wa La Liga huku tuzo ya kiungo bora imekwenda kwa Luka Modric.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *