Jeshi la Polisi mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa madai ya kuzidisha muda wakati akihutubia kwenye mkutano wake na wananchi jana.
Lema jana alifanya mkutano na wananchi wa jimbo la Arusha Mjini ambapo alizidisha muda wa mkutano wake jijini humo.
Polisi wamedai kuwa Lema alimaliza mkutano wake saa 12:7 jioni badala ya saa 12:00 kama ilivyo utaratibu.
Hivyo askari polisi walimzuia katika mzunguko wa barabara wa Mnara wa Saa (round about) kwa kusimamisha gari mbili (moja mbele na nyingine nyuma), kisha kuingia katika gari yake na kumuelekeza Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) mjini Arusha.
Mbunge huyo anashikiliwa na Polisi jijini humo kutokana na kosa hilo jijini Arusha la kuzidisha muda wa mkutano wake.