Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gigy Money amejibu madai ya taarifa za kurudiana na mzazi mwenzie Mo Jay baada ya kuonekana wakiwa pamoja na mtoto wao Mayra.

 

Gigy Money amekanusha hilo kwenye ‘Insta Story’ yake kwa kueleza hajarudiana na mtu hivyo watu wasidanganywe na trending za story hizo mitandaoni, kilichotokea ni Mayra alikuwa anaumwa na baba yake kaenda kumuona.

 

Hiyo inakuja baada ya msanii huyo kuonekana akiwa na baba mtoto wake huyo ambaye ni mtangazaji kituo cha radio cha Clouds FM.

Kupitia Instastory yake Gigy Money ameweka wazi kuwa hajarudiana na baba mtoto wake huyo ila alienda kumtembelea mtoto wao Mayra ambaye kwa sasa ni mgonjwa.

“Sijarudiana na mtu jamani, naona natrend huko wanawadanganya tu, Mayra anaumwa na baba yake kaja kumuona nimependa jinsi wamecoperate kwa hiyo sioni kama ni kosa, mniache”. comment ya Gigy Money

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *