Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford almaarufu Gigy Money amesema kuwa, asilimia kubwa ya watu wanaokesha kumsema vibaya mitandaoni kuwa anapenda kujichetua, hawayajui maisha.

Gigy Money amesema kuwa maisha ni fumbo zito mno na kila mtu ana lake hivyo hao wanaosema anajichetua mitandaoni, waache waendelee kuongea kwa sababu kujichetua kwake ndiyo kunamfanya yeye na familia yake waweze kuingiza tonge mdomoni.

Kuna watu wanakaa kusema wenzao utadhani wao ni malaika, kwamba hawana kasoro hata moja, wengi wanaonisema vibaya mitandaoni bado hawajajua nini maana ya maisha.

Pia amesema kuwa kuna muda huwa najichetua mitandaoni ili kujipa tu furaha ambayo nimeoikosa kwa watu ninaowategemea, lakini kujichetua kwangu pia kunanipa madili mengi ya pesa ambayo yananisaidia mimi na mwanangu,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *