Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gigy Money amefungiwa na baraza la sanaa Tanzania (Basata) kutokujihusisha na shughuli zozote za kimuziki kwa muda wa miezi sita.
Taarifa ya Basata imeeleza kua hatua hiyo zimechukuliwa baada ya msanii husika kuvaa nguo zisizo na maadili katika tamasha la Wasafi Tumewasha Tour lililofanyika mkoani Dodoma 1 january 2021 na kua kukiuka kanuni za kimaadili.
Baraza limejiridhisha kua alikiuka maadili ya kazi za sanaa kwenye Tamasha husika na kukiuka kifungu 4(L) cha sheria No 23 ya mwaka 1984 (Re: 2002), kanuni 25(6) (9) ya kanuni za Baraza za mwaka GNN.43/2018 na taratibu za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini.
Katika maelezo ya barua hiyo Baraza limeweka wazi kua mara kadhaa Gigy Money aliitwa na kuonywa kwa vitendo vya ukiukwaji wa maadili na aliahidi kutorudia tena.
Kutokana na ukiukaji huo wa maadili Baraza limemfungia kujihusisha na shughuli za sanaa kwa Kipindi cha miezi sita (6) ndani na nj’e ya nchi na kulipa faini ya shilingi za kitanzania Millioni moja(1,000,000/=).