Kiungo wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs amesema kuwa ligi kuu nchini Uingereza imejaa makocha wengi wa kigeni ambapo Waingereza hawapewi nafasi.
Giggs mwenye umri wa miaka 43 ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Manchester United chini ya kocha Louis Van Gaal misimu miwili.
Kauli hiyo ya Giggs imekuja kufuatia klabu saba pekee kati ya 20 zinazocheza ligi hiyo ndiyo zinafundishwa na makocha wa Waingereza.
Giggs amesema hana haraka kurejelea kazi ya ukocha huku akitoa sifa kwa kocha Paul Clement wa Swansea City ni ishara wakufunzi Waingereza wanaweza kufanikiwa.
Ligini kwa sasa, klabu saba zilizo juu kwenye msiamamo wa ligi hiyo zipo chini ya makocha kutoka nje.
Timu ambayo ipo juu zaidi inayofundishwa na Mwingereza ni West Brom ambao wamo chini ya Tony Pulis kutoka Wales.