Mchezaji soka wa zamani wa Liberia, George Weah anatarajiwa kuwa miongoni mwa wagombea kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu wa Liberia utakaofanyika Okoba 10 mwaka huu.

Weah ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa dunia anaingia kwenye kinyang’anyiro hiko kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 2005 na kushindwa na rais wa sasa Ellen Johnson ambaye muda wake wa uongozi unamalizika mwaka huu.

Jumla ya wagombea 20 wamejitokeza kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuwania nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa nchi  hiyo utakaofanyika mwaka huu.

Weah anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa sana kwa wananchi wa Liberia kutokana na umaarufu wake katika soka pamoja na ukomavu wa alionao kwenye siasa pamoja na uharakati za haki za binadamu.

Weah atakuwa akiwania kiti hicho huku makamu wake akiwa ni Jewel Howard Taylor, 54, ambaye ni mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo Charles Taylor.

Wagombea wengine waliotajwa ni Prince Johnson, MacDella Cooper, Makamu wa sasa wa rais, Joseph Boakai na wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *