Nchi ya Gambia imetangaza nia yake ya kujiondoa mahakama ya kimataifa ya makosa ya kiarifu ya kivita ICC iliyopo nchini Uholanzi.
Gambia kama ikijiondoa mahakama hiyo itakuwa taifa la tatu barani Afrika kujitenga na mkataba wa Roma uliounda mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.
Tayari Burundi na Afrika Kusini zimetangaza kujitoa kutoka kwenye mahakama hiyo.
Waziri wa mawasiliano ya taifa hilo, Sheriff Bojang amesema mahakama hiyo inatumika kuwanyanyasa Waafrika.
Fatou Bensouda ambaye ni mwendesha mshataka wa mahakama hiyo ni raia wa Gambia.