Muigizaji nyota wa Bongo movie, Salim Ahmed ‘Gabo’ amesema tuzo ni muhimu kwa wasanii kwa kuwa ni kipimo ambacho kinapima mafanikio ya msanii husika kutoakana na kushiriki kwenye tuzo husika.
Muigizaji huyo ameyasema hayo baada ya baadhi ya mastaa nchini kuzipotezea tuzo mpya zilizoanzishwa na East Africa Television ‘EATV Awards’ zitakazofanyika mwezi ujao katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Muigizaji huyo anawania tuzo ya muigizaji bora wa kiume katika tuzo hizo ambazo ni kwa mara ya kwanza zinafanyika nchini na kushirikisha wasanii wa muziki pamoja na wasanii wa filamu katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Gabo amesema hatua ya kuongezeka kwa tuzo nchini kunasaidia kukuza sanaa ya Tanzania kutokana na kuthaminiwa kutokana na kazi yako ya sanaa.
Kwa upande mwingine Gabo Zigamba akusita kuwashukuru waandaaji wa tuzo hizo ambao ni EATV kwa kuthamini michango ya wasanii na kuinua sanaa ya filamu na muziki katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Pia muigizaji huyo amesema huwenda ugeni wa tuzo hizo ndio kitu kingine kilichofanya mastaa wengi kutokuwa na mwamko zaidi wa kushiriki.
Gambo ni muigizaji nyota nchini ambaye alishawahi kushinda baadhi ya tuzo nchini kutokana na uigizaji wake kuwavutia watu na kwasasa anatamba na filamu yake inayojulikana kama Safari ya Gwalu.