Muigizaji wa Bongo Movie, Gabo Zigamba amesema kuwa sababu iliyochangia kushuka kwa Bongo Movie ni kutokuwa na soko rasmi la kuuza kazi zao pamoja na radha ya movie kupungua kwa watazamaji.

Gabo amesema hayo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na kituo cha radio cha EFM kwenye kipengele cha mada mezani ambapo leo kilikuwa kinaongelea sababu ya kushuka kwa soko la filamu nchini.

Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa wanaandaa movie kwa gharama kubwa lakini wanapopeleka kazi zao  sokoni wanapangia bei ya kuuza licha ya wao kuaanda kwa bajeti kubwa pindi wanapotengeza movie hizo.

Pia Gabo ameongeza kwa kusema kuwa filamu imekosa mtu wa kuzitetea pindi inapotokea tatizo la kushuka kwa soko lake kama kipindi hiki huku akiwataja COSOTA pamoja na BASATA ambao ndiyo wahusika wa filamu nchini.

Naye Muigizaji Batuli amesema sababu ya soko la filamu kushuka ni waigizaji wamekosa ubunifu kuandaa kitu kipya na wanapenda sana kukopi kazi za wasanii wa nje huku wakishindwa kufanya kazi zao wenyewe.

Pia Batuli amesema kuwa sababu nyingine ya kushuka ka soko la filamu nchini ni kutokana na kutosapoti wasanii wapya pamoja na kukua kwa tamthilia nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *