Muigizaji wa Bongo Movie, Gabo Zigamba amesema kuwa kudai ameamua kujitolea kufa na kupona ili kunusuru tasnia ya filamu isonge mbele kwa kutumia Teknolojia ya simu ambayo itawasaidia Watanzania kupata filamu bure na kwa urahisi.
Gabo amedai hayo wakati akizindua filamu yake ya ‘Kisogo’ kwamba ameamua kutoa sehemu ya maisha yake ili kuikomboa tasnia ya filamu ambayo imeonyesha kupoteza imani kwa mashabiki wa filamu nchini Tanzania kwa kutumia akili alizojaaliwa pamoja na kipaji chake kwa kadri atakavyopatiwa ushirikiano.
Aliongeza,”Kwa sasa filamu fupi zitapatikana kupitia mtandao wa Uhondo na kila mtu mwenye simu ya mkononi ataweza kuzipata, sehemu ya 1 bure na sehemu ya pili itakuwa ikichangiwa pesa kidogo ili kuweza kuzalisha kazi nyingi zaidi.
Pia amesema kuwa malengo ya kufanya hivyo ni ili kila mtanzania aangalie filamu hizo na baadaye mambo yakikaa sawa zitakuwa zikipatikana bure kabisa.
Muigizaji huyo amezindua filamu yake hiyo akiwa na muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu.