Aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Furguson amesema kuwa klabu hiyo sasa imeanza kuimarika chini ya kocha, Jose Mourinho ila bahati tu wamekosa lakini wangeweza kukabiliana vilivyo na Chelsea kwenye mbio za ubingwa.
Ferguson mwenye umri wa miaka 75 alistaafu kama kazi ya ukocha mwaka 2013 lakini bado ana uhusiano wa karibu na klabu hiyo ya Old Trafford kwani huhudhuria michezo yake mingi pindi timu hiyo inapocheza.
Ferguson pia alielezea kwa nini rekodi ya ufungaji magoli ya mshambuliaji wa Manchester united Wayne rooney haitavunjwa na mchezaji yoyote yule karibuni.
Jose Mourinho ni kocha wa tatu kuiongoza klabu ya Manchester United tangu Ferguson kustaafu alipochukua nafasi ya Louis van Gaal mwezi Mei mwaka jana.
Mourinho alishinda mechi tatu zake za kwanza akiwa na Manchester United, alishinda alama sita pekee kutoka kwa mechi saba za Ligi kuu zilizofuata.