Muigizaji maarufu wa Marekani, Sylvester Stallone amekubali kufanyiwa marudio kwa filamu yake ya Rambo kwa kihindi.
Muigizaji huyo amesema kuwa itakuwa vizuri kwa filamu hiyo kurudiwa tena nchini India kutokana na ubora wa filamu hiyo iliyofanya vizuri miaka ya nyuma.
Kwa upande wa mkurugenzi wa filamu hiyo, Sid Anand ameambia mashabiki wa filamu hiyo kuwa haitokuwa na nyimbo na kucheza dansi kama ilivyozoeleka kwa filamu za Bollywood .
Filamu hiyo itazinduliwa katika maonyesho ya filamu ya Cannes lakini bado filamu hiyo haijarekodiwa ambapo itaanza kurekodiwa mwaka huu.
Muigizaji nyota wa India, Tiger Shroff ndiye atakayeigiza kama Rambo kwenye filamu hiyo inayotarajiwa kukonga nyoyo za watu.
Kuhusu uamuzi wake wa kuizindua filamu hiyo Cannes, Anand amesema: “Rambo anatambulika katika kila sehemu ya duniani. Kwahivyo ni muhimu kuizundua filamu hiyo katika eneo kuu la utengenezaji Filamu.”
Amesema amepata msukumo wa kuitengeneza filamu hiyo Kihindi kutokana na uzito wa muigizaji mkuu “muigizaji wa kikweli wa kupigana aliye na moyo mkubwa”, aliyefufuliwa na Stallone.
Anand amesema ameipangilia filamu hiyo kwa namna ambavyo itakuwa rahisi kueleweka India lakini ameonya huenda ikazusha mzozo kama ilivyokuwa kwa Rambo First Blood katika miaka ya 80.