Filamu ya ‘Slay’ aliyocheza Mtanzania, Idris Sultan na wenzake kutoka nchi mbalimbali Afrika imeweza kurejea kwenye mtandao wa Netflix tangu iondolewe Mei 2, 2021.
Filamu hiyo iliweka Netflix Machi 26 mwaka huu, huku Idris akiweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza nchini kuingiza filamu kwenye mtandao huo mkubwa duniani kwa mauzo ya filamu.
Sababu ya kutolewa ni kutokana na kukiuka taratibu za hakimiliki ambapo filamu hiyo imetumia wimbo uitwao ‘All For You’ wa msanii, Wendy Shay kutoka Ghana bila makubaliano yoyote.
Baada ya suala hilo kumalizika ndani ya miezi, Netflix wameirejesha filamu hiyo kwenye jukwaa lake.
Ukiachana na Idris, filamu hiyo ina wakali kama Tumi Morike, Ramsey Nouah, Fabian Adeoye Lojede, Enhle Mbali, Amanda Du-Pont, Lillian Dube na wengineo.