Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi mkoani Simiyu wameandamana kupinga Mkuu wa Shule yao, Deus Toga kuhamishwa.

Wakati wa maandamano hayo yaliyofanyika wanafunzi hao wapatao 600, walifunga barabara kuu ya Bariadi – Lamadi.

Shughuli mbalimbali za  jamii mjini Bariadi zilisimama kwa zaidi ya saa mbili kwa kuwa hakukuwa na utulivu.

Taarifa zilizopatikana zinasema   wanafunzi hao waliandamana wakipinga Mwalimu Toga kuhamishiwa katika Shule ya Sekondari Giriku.

Wanafunzi walianza kuandamana kuelekea ofisi ya Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Merkzedek Humbe, ambaye ndiye aliyemhamisha Mwalimu Toga.

Wakati wakielekea ofisini kwa mkurugenzi huyo, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliwadhibiti kabla hawajafika walikokuwa wakielekea.

Taarifa zinasema   walipozuiwa kuelekea ofisini kwa mkurugenzi, walibadili mwelekeo na kuelekea ofisini kwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu ili wakapeleke malalamiko yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *