Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Serikali ya Tanzania wamesaini makubaliano ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali  Gaudence Milanzi, amesema  mpango huo utagharimu kiasi cha Sh milioni 280 ambazo zimetolewa na FAO kufanya utafiti wa kuongezea takwimu ambazo zitaboresha Sera ya Misitu ya Taifa  ili iweze kufikia hadhi ya kimataifa.

Amesema hatua hiyo imekuja kutokana na Sera ya Misitu ya Taifa ya mwaka 1998 inayotumika hivi sasa kupitwa na wakati yakiwemo mabadiliko ya kiuchumi, kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero, alisema mradi huo utasaidia wananchi wengi kushiriki na kutoa mawazo mengi kuhusiana na Sera ya Misitu ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo watumishi kuweza kukusanya taarifa nyingi ili ziwezeshe kuboresha sera kupitia tafiti.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *