Mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny aitwae Fahyvanny ameweka wazi kuwa amechoka kuvumilia penzi la staa huyo kutokana na matukio anayokutana nayo kila siku

Fahymah ameenda mbali kwa kumwambia Rayvanny kuwa amechangia kwa asilimia kubwa kuivunja familia yake na pia ameshindwa kuiheshimisha familia mbele ya jamii kutokana na skendo anazokutana nazo kila siku.

Hivyo kwa kuandika hayo Fahymah amesema kuwa ameachana rasmi na Staa huyo kutokana na mamabo yake anayofanya kwa jamii.

Kwa habari za chini chini zinadai kuwa Rayvanny amekufa ameoza kwa Paula kitu ambacho kimesababisha migogoro kwenye familia yake.

Pamoja na Fahymah kujua hilo amekuwa akipata utetezi kutoka kwa Rayvanny uliomfanya aendelee kumvumilia ila kwa sasa imetosha ameamua kuachana na mwanamuziki huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *