Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya IPTL ya kuongezewa muda wa leseni yake ya biashara kwa miezi 55 ili iendelee kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO.
Mbali na kusitisha mchakato huo, EWURA imesitisha pia upokeaji wa maoni kutoka kwa umma na wadau mbalimbali kuhusu kusudio lake la kuiongezea muda wa kufanyakazi nchini Kampuni ya IPT.
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri mkuuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Felix Ngamlagosi kuanzia jana tarehe 11 Juni, 2017.
Maamuzi haya yamekuja siku mbili baada ya habari za kampuni ya IPTL kuongezewa mkataba wa uzalishaji umeme.