Muigizaji wa Bongo Mpvie, Ester Kiama amefunguka na kusema kuwa anafunga kwaresma siku 40 kwa ajili ya ombi lake la kupata mtoto litimie.

Mwanadada huyo amesema kuwa kkwa kipindi hiki cha mfungo wa kwaresma amekuwa akifunga siku zote 40 huku hitaji lake kubwa ikiwa ni kuombea kupata mtoto hasa mtoto wa kike.

Kiama amesema kuwa amejitahidi sana kufungwa kwa sababu anaona kabisa kwa sasa anahitaji kupata mtoto na ameamua kumshirikisha mungu kwa sababu anajua kuwa hakuna kinachoshindikana kwa hilo.

Pia amesema kuwa Katika kipindi hiki cha kwaresma, nimeamua kufunga huku ombi langu kubwa ikiwa na kumuomba mungu anijalie niweze kupata mtoto wa kike maana ndio hitaji la moyo wangu na ndio maana nimejitahidi kufunga siku zote kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Kipindi hiki cha mwezi wa kwaresma ambao wakristo wengi wamekuwa wakifungwa kwa ajili ya kuheshimu mateso ya yesu kristo na kufunga hili kuomba mahitaji yao kukamilika.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *