Dada wa Diamond Platnumz, Esma Platnumz amesema kuwa, hakuna uhasama wowote kati ya kaka huyo na aliyekuwa msanii wake, Harmonize au Konde Boy Mjeshi.

Esma ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii amesema kuwa, mashabiki ndiyo wamekuwa wakitengeneza bifu kati ya wasanii hao wawili ilihali kiuhalisia hanana tatizo. “Ninyi ndiyo mnawagombanisha.

Siyo wao. Wao wako sawa kabisa,” amesema Esma. Mama huyo wa watoto wawili anamtaja Harmonize kama mtoto wa Diamond na kusema kaka’ke hawezi kubishana naye.

Esma anasema kwamba familia ya Wasafi inafurahia mafanikio ya Harmonize kwa kuwa aliwahi kuwa mmojawao.

“Tunatamani kumuona Harmonize akipiga hatua kwa sababu ni mtu wetu, ametoka kwetu. Tunafurahi akiwa anazidi kupiga hatua. Hakuna kinachotuuma kwa kuwa ni mtu wetu. Diamond hawezi kujibizana na mtoto wake,” anasema Esma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *