Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Enock Bella amesaini mkataba na kampuni ya Chakor Music Group ya nchini Burundi itakayokuwa ikisimamia kazi zake za muziki.
Meneja wa Chakor Music, Kenth amesema kampuni yao ina wasanii wengi wa Afrika Mashariki, lakini wameingia Tanzania kujitanua na ku-push muziki wa Bongo Fleva.
“Tumeingia Tanzania kusaka wasanii wenye vipaji tunaoweza kuwasimamia, tukanona Enock ana uwezo mkubwa, kazi zake tumezifuatilia ana sauti nzuri, anajua kuimba na anajua muziki, hivyo tunaamini tutafika naye mbali.
Kwa upande wa Enock ambaye amesaini mkataba huo wa miaka mitatu ameshukuru kupata management mpya ya kumuongoza kimuziki baada ya kundi lao la Yamoto Band kuvunjika.
Kwa upande wake Enock Bella amesema kuwa “Sikujua kama kazi ninayoifanya inapenya hadi mbali.
Pia amesema kuwa Namshukuru Mungu nimepata management, nawashukuru pia Chakor Music kwa kuona kipaji na mchango wangu kwenye tasnia ya muziki. Naamini sasa nitafanya muziki ufike mbali zaidi ya vile nilivyokuwa nikifanya mwanzo, mkataba ni mzuri, tukishirikiana kwa pamoja tutafika pale tunapopataka,”.