Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Enock Bella amefunguka na kukanusha kuhusu tuhuma kuwa wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band kwa sasa hawaelewani.
Eneck Bella amesema kuwa hakuna ugomvi wowote kati yao na ipo siku watu watawasikia wakishirikiana katika ngoma tofauti tofauti.
“Ukifika muda tutachukua ngoma za Yamoto Band na kupeleka watu, usishangae kusikia ngoma yangu na Aslay, pia usingae kusikia ngoma mimi na Beka, pia usishangae kusikia ngoma na Maromboso, bado upendo wetu upo pale pale.
Hadi kufikia sasa wasanii wote waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band wametoa kazi zao binafsi, Aslay anaongoza kuwa na nyimbo nyingi Zaidi kuliko wenzake.