Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Enock Bella amesema kuwa hawezi kuwalaumu wenzake kutompatia sapoti kutokana na kwamba kwa sasa kila mtu ana maisha yake na washakuwa wakubwa.

Enock Bella amethibitisha kuwa kwenye album mpya ya Beka Fleva kuna ngoma amefanya naye na ni ngoma kali kiasi kwamba wapenzi wa muziki wataipokea vizuri.

Alipogusiwa uhusu kufanya kazi na Mbosso pamoja na Aslay amedai kuwa nyimbo na Mbosso ni suala la muda tu lakini lazima itoke hiyo ni lazima kwahiyo wapenzi wa muziki wasubiri kwa hamu kazi yake na Mbosso.

Kuhusu Aslay amedai yupo bize sana kuna nyimbo alimtumia lakini kutokana na kubanwa hajafanikiwa kufanya naye kazi.

Msanii huyo ambaye ametoa nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la NDOA yenye miondoko ya singeli ambayo imeanza kufanya vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *