Eneo la uwanja ambalo Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameipa klabu hiyo lina mgogoro.

Manji juzi ametoa eneo la hekari 715 lililo ufukweni mwa Bahari ya Hindi, Gezeulole, Kigamboni kwa ajili ya kujenga uwanja.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam zinasema eneo hilo lipo kwenye mgogoro wa ardhi na Kampuni ya mafuta ya Lake Oil.

Eneo hilo si lote mali ya Manji bali kuna sehemu nyingine inamilikiwa na Lake Oil.

Mmoja wa wakurugenzi wa Lake Oil, Khalid Hassan amesema ameshangazwa kuona Yanga wamekabidhiwa eneo lote hilo wakati kuna sehemu yao pia.

Juzi, Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo chini ya Fatma Karume walikabidhiwa eneo litakalojengwa uwanja wa Yanga lililopo Gezaulole, Kigamboni.

Eneo hilo ambalo Manji inadaiwa aliuziwa na Shirika la Taifa la Kilimo na Chakula (NAFCO), kwa upande wa Lake Oil walidai kuwa hawajauziwa na Nafco wameuziwa na mtu mwingine ambaye hata hivyo hawakutaka kumtaja na pia kuweka wazi ukubwa wa eneo ambalo wanadai wanalimiliki.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa Manji baada ya kuuziwa eneo hilo aliliacha kwa muda mrefu bila kuliendeleza ndipo watu wengine wakavamia na hata kuuza baadhi ya maeneo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *