Eneo la jengo la Billicanas lililokuwa likimilikiwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe linatarajiwa kujengwa maduka ya kisasa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) baada ya kulichukua jengo hilo.

Jengo la Billicanas lilibomolewa na shirika hilo mwishoni mwa wiki baada Mbowe kuondolewa mwanzoni mwa Septemba mwaka jana kutokana na kushindwa kulipa deni la Sh bilioni 1.3 ambazo zilikuwa pango ya miaka 20.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, alisema ujenzi wa maduka hayo madogo madogo ya kisasa yatakayokuwa katika ghorofa tano, unatarajia kuanza mwakani baada ya kukamilika kwa taratibu za kutafuta mzabuni.

Mchechu amesema kuwa mbali ya jengo la Billicanas, kuna majengo mengine manne yanayomilikiwa na shirika hilo yatabomolewa ili kukamilisha ujenzi huo.

Amesisitiza kuwa ubomoaji wa majengo hayo utafanyika ndani ya mwezi huu ili kuweza kuharakisha ujenzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *