Mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye alikuwa Yamoto Band, Enock Bella amekanusha taarifa kwamba Aslay alitoweka na daftari la nyimbo za Yamoto Band.

Taarifa hizo zilisema kuwa baada ya kuondoka Yamoto na kuwa na nyimbo nzuri kila siku ni kwa sababu wakati anaondoka Yamoto band aliiba daftari la nyimbo la Yamoto ambalo alishirikiana na wenzake kuandika.

Aslay ni mmoja Kati ya wasanii anayefanya vizuri sana kwa hivi sasa mafanikio anayopata ni wasanii wachache wanaoweza kufikia ukitegemea kwa mtindo wake wa kutoa nyimbo kila baada ya muda mfupi.

Lakini mafanikio Kama haya lazima yaje na changamoto kadhaa kwa upande wa Aslay changamoto hiyo ni bendi yake ya zamani ya Yamoto Band iliyovunjika miezi michache iliyopita na kupelekea vijana waliokuwa wanaunda bendi hiyo kutengana.

Enock Bell ambaye alikuwa kwenye bendi ya Yamoto na Aslay amefungukia tuhuma hizo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha  East Africa:

Enock alikataa tuhuma hizo na kudai kuwa sababu pekee watu wanasambaza habari hizo ni baada ya kuona Aslay anatoa nyimbo kali kila siku lakini amedai hicho ni kipaji chake tu na sio wizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *