Mwanamuziki wa Hip Hop nchini, Edu Boy amedai kukerwa na kitendo cha Dogo Janja kumuita yeye mtoto mdogo na kumtaka atengue kauli yake hiyo kwani kuoa kwake kusimfanye awe na dharau kwa wengine.
Kauli hiyo ya Edu Boy imekuja kufuatia Dogo Janja kumuita mtoto ambae anahitaji kuisoma vizuri game ya muziki ili aweze kukua nayo hivyo hawezi kubishana nae.
Dogo Janja alitoa kauli hiyo dhidi ya Edu Boy baada ya kuchanwa kwenye wimbo mpya wa Edu kwenye mstari uliosema ‘Kwa unafki Dogo Janja anaongoza’.
Edu Boy amesema kuwa anamtaka Dogo Janja atengue kauli yake ya kumuita mtoto mdogo kwasababu umri wao ni sawa ila tu Dogo Janja amewahi kuoa.
Kwa upande mwingine, Edu Boy amemtaka Dogo Janja awe makini na ndoa yake ili mabomu yakija kurupuka afe mwenyewe kwenye ndoa yake.