Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutokea pande za Mwanza, Edu Boy amesema kuwa Dogo Janja ameolewa na ndo maana anaona wenzake wadogo hivyo apambane na ndoa yake.
Edu Boy amesema kinachomsumbua Dogo Janja ni kwamba ameolewa na hajaoa, huenda baada ya yeye kufunga ndoa anahisi kwamba kila kitu kipo sawa kwake na kuwaona wasanii wenzake wadogo kiumri na hata kimaisha.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa Dogo Janja ni mdogo sana kwake hivyo hana uwezo wa kumshika na kumpiga vibao kama mdogo wake.
Pia amefunguka kuwa anasikia Stamina anamtafuta hivyo aende tu kwenye maeneo ambayo anapatikana kama studio za Mona Ganster atamkuta wamalizane.