Mchekeshaji maarufu nchini, Ebitoke amefunguka na kusisitiza kuwa yeye na staa wa Bongo Fleva, Ben Pol wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi na sio kiki kama wengi wanavyosema.

Tangu walivyotangaza kuwa wapo kwenye mahusiano Kumekuwa na tetesi nyingi huku watu wengi wakidai kuwa hawana mahusiano yoyote bali wanatafuta tu kiki ili Ben Pol auze mziki wake na Ebitoke ajulikane kwa komedi.

Lakini mara kwa mara Ebitoke amekuwa akisisitiza kuwa wenyewe wapo kwenye mahusiano na amekuwa akisisitiza kuwa anampenda sana Ben Pol ingawa inasemekana ana mpenzi mwingine.

Lakini pia Ebitoke amefungukia tetesi zinazomzunguka mchekeshaji mwenzake Mama Ashura ambapo inadaiwa Ebitoke alimuibia bwana, jambo ambalo amelikataa na kusema kuwa Mama Ashura yupo anatengeneza kazi zaidi siku si nyingi ataonekana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *