Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amesema kila mwanamke anapenda kuwa na ngozi nzuri lakini kutumia madawa ya vipodozi ili kujichubua ni utumwa na kuna muda ukifika unaanza kujichukia.

Dayna Nyange amejibu baada ya Amber Lulu kuweka wazi kwamba anataka kujichubua ili kuwa mweupe.

Ikumbuke Dayne Nyange ni mmoja waliowahi kujichubua kwa kutumia vipodozi vikali kitu ambacho hatamani kukifanya tena.

Siku zilizopita mwanamuziki Amber Lulu alisema kuwa anatamani sana weupe ila aonekane mrembo mbele ya jamaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *