Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Dully Sykes amesema kuwa hawezi kutoa album kabisa kwasababu anaamini hazina faida kama zamani ambapo zilikuwa zinalipa zaidi kulinganisha na siku hizi.
Mkali huyo wa Inde amesema album zilikuwa zinaingiza pesa kipindi kile yeye anaanza kufanya muziki lakini siyo kwa kipindi hiki ambapo hazilipi hata kidogo mpaka kupelekea wasanii wengi kutoa single tu badala ya albam.
Dully amesema kuwa “Album zilikuwa zina dili kipindi kile mimi naanza muziki, lakini siku hizi ujanja ujanja umekuwa mwingi sana ndiyo mana tumesusa kutoa albamu, bora tutoe nyimbo tu.
Mwanamuziki huyo ameendelea kwa kusema kuwa hawezi kutoa album labda mpaka asikie maharamia wa kazi za sanaa wamedhibitiwa vya kutosha na hapo ndiyo ataanza kutoa albam lakini si kwa kipindi hiki.
Dully Sykes kwasasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Inde’ aliomshirikisha Harmomize kutoka WCB na umeonekana kufanya vizuri masikioni mwa watu mara tu baada ya kutoka hivi karibuni.
Dully Sykes ni mwanamuziki mkongwe sana katika anga ya muziki wa Bongo fleva ambapo hapo awali alikuwa anatoa albam lakini kwasasa amesitisha baada ya kuona ubabaishaji mwingi katika soko la albamu hizo.