Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amesema kuwa anatarajia kuubuluza mahakamani mtandao maarufu wa simu za mkononi nchini kwa madai kwamba umeshindwa kulinda nyaraka zake muhimu.

Dully amesema kuwa, mtandao huo umesababisha matapeli kutumia laini yake ya simu kufanya utapeli kwa watu wake mbalimbali.

Amesema kuwa “Kuna mtu ame-renew laini yangu, akapewa ushirikiano mkubwa na kampuni hiyo ya simu, aka-hack’ facebook yangu kisha akawaomba watu pesa na picha za utupu kwa wanawake, lazima niushtaki mtandao huu kwani unahusika,”.

Dully Sykes ameilalamikia kampuni moja wapo ya simu nchini na kusema kuwa kampuni hiyo imeweza kumsaidia tapeli mmoja jijini kuweza ku-renew laini yake ya simu na kuweza kuitumia kwa watu wake wa karibu kwa kuwaomba ela , kuwatapeli na hata kuwadhalilisha baadhi ya wanawake kwa kuwaomba picha za utupu.

Dully amesema kuwa linakuja suala la kuwashughulikiwa waalifu hao baadhi ya kampuni za simu wanakuwa wanashindwa kufanya udhibiti huo wa taarifa za watu wengine kuvuja katika mitandao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *