Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amesema wimbo wake hunifahamu ina historia ya ukweli kwa sababu kuna mwanamke alikuwa analazimisha kuwa naye kwenye mahusiano walipokutana Manyoni Singida.

“Historia ya Hunifahamu ni ya ukweli, ilianzia Manyoni Singida ikaja Dar yule msichana sasa ni marehemu alikuwa anaitwa Zamzam.

Dully amesema kuwa kuna jambo lilitokea huko siwezi kulizungumzia kuhusiana na upoteaji wa simu ambao nilienda na wenzangu”.

“Baada ya hapo yule msichana alirudi akaniambia haitaki tena ile simu wala hana mpango nayo, akasema anahitaji kuwa na mimi, sasa kwa kipindi kile nilikuwa na mwanamke naishi naye, nikamwambia asije kwangu ataniharibia mapenzi yangu”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *