Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dudubaya amesema kuwa kwasasa ameachana na matumizi ya pombe kwani pombe ilikuwa inamuweka mbali na Mungu.

Dudubaya amesema amekuwa akitumia pombe kali kwa muda mrefu sana kitu  ambacho hakupata faida yeyote na pombe hizo na mwisho wa siku zimemfanya kuishi maisha ya ajabu ambayo hayampendezi mungu na wakatu mwingine kushindwa hata kwenda kwenye nyumba za ibada.

Mwanamuziki huyo alitamba miaka ya nyuma amesema kwa sasa anawaepuka marafiki wote ambao wamekuwa wakimshawishi kutumia pombe kali kwani ni marafiki ambao sio wazuri na amekuwa nao kwenye maisha yake kwa mda mrefu lakini hajaona faida yeyote aliyopata zidi ya kuwa mlevi wa kupindukia.

Pia Dudubaya amemalizia kwa kusema mwaka 2018 ni mwaka ambao amejipanga kufanya vizuri kwenye sanaa yake kwa kuandaa nyimbo na video nzuri na kusema atahakikisha anaongeza mahudhurio yake katika nyumba za ibada ili kuweza kujiweka sehemu nzuri ya kiimani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *