Mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba amekataa kuichezea klabu yake ya Montreal Impact baada ya kuambiwa hataanzishwa kwenye mechi dhidi ya dhidi ya Toronto.

Drogba mwenye umri wa miaka 38 hakuwepo katika uwanja wa michezo wa Saputo ambapo Impact ilipata sare ya 2-2 na hivyobasi kuweza kufuzu kwa michuano ya ligi ya Marekani.

Montreal hapo awali ilikuwa imesema kuwa Drogba alikuwa anauguza jeraha la mgongo na hivyobasi asingeweza kucheza.

Kocha wa klabu hiyo Mauro Biello amesema hakukubali kwamba angechezeshwa kama mchezaji wa ziada na mwishowe hakutaka kushirikishwa katika kikosi cha watu 18.

Pia kocha huyo aliongezea kwa kusema kuwa alikuwa na tatizo katika mgongo wake lakini alikuwa anaweza kucheza.

Drogba ambaye aliondoka Chelsea mwezi Julai 2015 amekuwa akitumiwa kama mchezaji wa akiba katika mechi mbili kati ya nne.

Toka ajiunge na klabu hiyo Drogba amfunga mabao 10 katika mechi 21 msimu huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *