Mtangazaji wa E-FM, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ amefunguka na kusema kuwa hapendi mapenzi ya Lulu Diva na Rich Mavoko ambaye ni kaka yake.

Dokii amesema kuwa hajawahi kumpenda mwanamuziki Lulu Diva hata kidogo na wala hafikirii kama anaweza kuwa mke bora kwa kaka yake huyo.

Dokii ambaye ni muigizaji mkongwe nchini amesema kuwa yupo tayari watu wamseme kuwa yeye mkorofi lakini ahakikishe kaka yake hamuoi Lulu Diva.

Pia Dokii amesema kuwa sababu inayomfanya asipende Lulu Diva kuolewa na kaka yake huyo ni kutokana na tabia ya Lulu Diva kuwa siyo nzuri kutokana na tabia ya kutoka na wanaume wengi maarufu nchini.

Alipoulizwa kama anatumia ‘ndumba’ kumtengeneza Mavoko hadi kumsahau msichana aliyezaa naye, alisema si kweli kwani mwanamke anayejiamini hawezi kutumia ushirikina katika kumdhibiti mwanaume.

Kwa upande wa Lulu Diva hadi sasa hivi anasema kuwa  hajawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na Rich Mavoko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *