Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Dogo Janja amesema kuwa wanatarajia kuhama nyumba waliyokuwa wakiishi na marehemu Agness Masogange wakidai kuwa hawatakuwa na amani.

Dogo Janja amesema kuwa watahama nyumba hilo kwasababu hawatakuwa na amani kutokana na kumbu kumbu ya kifo cha Masogange.

“Kwa kweli mimi na mke wangu hatuwezi tena kuendelea kuishi Makongo Juu kwenye ile nyumba maana kwetu itakuwa ni simanzi tuu, Masogange alikuwa ni mtu wetu wa karibu sana na tulikuwa tukifanya vitu vingi pamoja, pia mke wangu atakuwa na huzuni sana akiendelea kuishi pale,”.

Dogo Janja alisema kuwa hawawezi kuendelea kuishi hapo tena kwa sababu kwao itakuwa ni majonzi kila siku na hiyo ni kutokana na ukaribu waliokuwa nao kwa Masogange.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *