Msanii wa Hip Hop Bongo, Abdulaziz Chende maarufu kama Dogo Janja au Janjaro amefunguka na kusema kuwa kwasasa hana mpango wa mtoto bado sana maana anajipanga na hawezi kukurupuka.
Dogo Janja ambaye yupo chini ya Madee amesema kuwa bado hajapanga na mpenzi wake kupata mtoto japokuwa mipango hiyo ipo ila siku za baadae siyo kwasasa kwani unri wake bado mdogo.
Dogo Janja amesema kwa sasa wanakula bata kwanza wakiendelea kutathmini siku wakipata mtoto wao ataishije.
“Huwezi kuzaa kwa ajili ya watu, sina mpango wa kuwa na watoto zaidi ya watatu, nadhani wawili wananitosha, lazima nijipange kwanza kujua mwanangu ataishije nisije nikakurupukia kuzaa halafu mwanangu akateseka,” anasema Janjaro.
Dogo Janja yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo wa Arusha ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa jijini humo.