Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amewajia juu watu ambao bado wanaiponda ndoa yake na Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya.

Kauli hiyo ya Dogo Janja imekuja kufuatia baadhi ya watu kujaji ndoa yake na muigizaji huyo wa Bongo Movie.

Dogo Janja amedai kuwa amechoshwa na watu wote wanaomsema vibaya kuhusu ndoa yake katika mitandao ya kijamii.

Pia Dogo Janja amesema wimbo wake ya Wayu Wayu ni ujumbe kwa wale watu wote wanaomsema vibaya kwa kufunga ndoa na Uwoya.

Kwa upande mwingine Dogo Janja amesema kuwa mashabiki wanatakiwa kumsapoti kwenye kazi yake ya muziki lakini si kuingilia maisha yake binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *