Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutokea pande za Tip Top Connection, Dogo Janja amemchana mwanamuziki mwenzake, Edu Boy kutoakana na aina ya muziki wake wa kidis wanamuziki wenzake.

Edu Boy ni mwanamuziki ambaye aina yake ya uimbaji uwadiss wasanii wenzake katika mashairi yake.

Dogo Janja amesema kuwa anachokifanya mwanamuziki huyo ni utoto mtupu na kwamba hawezi kufaidika na lolote kutokana nyimbo zaina hiyo.

Pia Dogo Janja amesema kwamba msanii anapaswa kuimba kitu ambacho hata kizazi kijacho kikipata fursa ya kuskiliza nyimbo zao kitajifunza kitu kupitia mashairi ya msanii husika.

Dogo Janja ameendelea amesema kuwa mpaka sasa watu wanasikiliza nyimbo walizoimba wasanii wa zamani kama kina Mbaraka Mwinshehe kwa kuwa waliimba nyimbo zenye maadili na zenye ujumbe kwa jamii.

Dogo Janja amesema kuwa Edu Boy ni kama mdogo wake kwenye sanaa kwa kuwa amemkuta kwenye game ya muziki kitambo hivyo hawezi kumsumbua kwa mistari yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *