Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amekanusha tetesi zilizoenea kuwa aliwaogopa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ndiyo maana akaigiza kama ‘video queen’ katika video yake ya ‘Wayu Wayu’.
Dogo Janja amesema, anashangazwa na watu kuendelea kuongelea sababu za kujifanya mwanamke katika video hiyo huku wakihusisha na Basata, alisema alichokifanya ni sehemu ya kazi za sanaa katika kufikisha ujumbe kwa jamii.
Amesema kuwa “Hapana, siyo kwamba niliogopa Basata, ujue hauwezi kuwa mwanasanaa kama huwezi kuichezea sanaa, nilichofanya ni ubunifu tu,”.
Katika video hiyo, Dogo Janja anaonekana akiwa amejipodoa huku akiwa ndani ya mavazi ya kike mwanzo mwisho.