Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa ni kweli anayapenda mapenzi lakini sio kama amehama Jijini Dar Es Salaam na kwenda kuishi Arusha kwa mpenzi wake Quenlinna Totoo.
Dogo Janja amesema huonekana mara chache sana kwenye shughuli maalum ndiyo maana watu wanadai kama amehama kumfuata mpenzi wake
“Dar Es Salaam nipo sana ila huwezi jua nilipo, nitatokea kukiwa na ishu muhimu maana sipendi kuonekana hovyo lakini watu wangu wa mtaani wananiona kila siku.
Dogo janja ameongeza kwa kusema kuwa mapenzi hayajawahi kumteka ila anayapenda na akipenda huwa nipo karibu na mpenzi”.