Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja wamehojiwa na Jeshi la Polisi na kuachiwa wakituhumiwa kuwashawishi abiria wengine kukataa kufanya kipimo cha ugonjwa wa COVID-19.

Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Serikali, wenyeji wanaorejea na wageni kutoka nje wanatakiwa kuwasilisha kipimo kinachothibitisha hawana maambukizi ya Covid-19, huku wanaotoka nchi zenye maambukizi wakitakiwa kupimwa kwa kipimo maalum ambacho kitagharimu Dola 25 za Marekani, sawa na TSh. 57,500 kwa kila msafiri.

Dogo Janja aliyekuwa akitokea Afrika Kusini jana, alipinga kufanya kipimo hicho na kuitangazia dunia kupitia ukurasa wake wa twitter kwa kuandika

“Hii nchi Tanzania bado ina uonevu wa kishamba sana, sidhani kama mama yetu Rais Samia Suluhu anafahamu.. muda huu nafika uwanja wa ndege wa kimataifa nikitokea Afrika Kusini na Afrika Kusini huko nimepima na nina majibu ya corona lakini hawayataki wanataka hela kutupima upya.”

“Sasa ndugu zangu wa Tanzania mimi nina hela lakini sitoi hata kumi…, mniletee uji kituo nitakachokuwepo nikikosekana hewani shughulikeni na Polisi wa uwanja wa ndege.” aliandika Janjaro.

Kamanda wa Kikosi cha Viwanja vya Ndege Nchini, Jeremia Shila, amesema wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kama tuhuma zinazomkabili Dogo Janja ni za jinai ili wafikishwe Mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *