Kampuni ya Submarine Entertainment na ByStorm Film wameanza kutayarisha  makala (Documentary) inayohusu maisha ya aliyekuwa staa wa hip hop nchini Marekani, B.I.G Notoriuos.

Makala hiyo itakuwa inaelezea maisha halisi aliyokuwa anaishi staa huyo kwa kabla ya kufikwa na umauti miaka 20 iliyopita.

Documentary hiyo fupi itakayoitwa kwa jina la ‘One More Chance’ bado ijathibitisha itatoka lini ila maandalizi ya kutengeza imeshaanza.

Makala hiyo inatarajiwa kutatayarishwa na Emmett na Brendan Malloy huku mama yake B.I.G ‘Voletta Wallace’ atahusika kwenye documentary.

Kwa upande wake Mama yake B.I.G amesema kuwa anafuraha kuona muziki na maisiha ya mtoto wake bado yana nafasi kubwa kwenye muziki na maisha ya vijana wa sasa.

Submarine wamewahi kushika dili kubwa za maisha ya mastaa kama Nas kwenye Time Is Illmatic na Searching for Sugarman na wengine kibao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *