Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Marekani, DMX amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi Zaidi dola milioni 1.7 katikati ya mwaka 2002 na 2005.

Upande wa mashtaka uliomba afungwe miaka mitano jela ili iwe funzo kwa wasanii wengine wanaopenda kukwepa kodi, awali alitakiwa kufungwa miaka 40 jela.

Wakili wa DMX , Murray Richman alicheza muziki wa DMX mahakamani, wimbo “Slippin” ili jaji aelewe ugumu wa maisha aliopitia DMX Na ndio kilichopelekea staa huyu kupunguziwa adhabu.

Mahakamani jana Jiji Jed Rakoff  alisema  DMX ‘ni mtu mzuri anayefanya makosa makubwa kwenye maisha yake, yeye mwenyewe ndio adui yake namba moja’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *