Baada ya kuteuliwa kuwa Balozi, Dkt Abdalah Posi ambaye alikuwa mbunge wa kuteuliwa amemuandikia barua ya kujiuzuru nafasi hiyo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.
Dkt Abdalah Posi ambaye alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa akishughulikia Ulemavu.
Rais Magufuli alimteua Dkt. Possi kuwa balozi katika kituo atakachopangiwa kazi baadaye ambapo kwa sasa bado ajapangia kituo hiko.
Spika Ndugai amesema kufuatia barua hiyo ya kujiuzulu ubunge ya Dk Possi, aliyoipokea Januari 20, mwaka huu iliiyozingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 67 (1) (g) na Ibara ya 149, amemwandikia Rais John Magufuli kuwa sasa wabunge wa kuteuliwa na Rais waliopo ni saba na nafasi zilizo wazi ni tatu.
Kutokana na uteuzi huo nafasi ya Naibu Waziri (Ulemavu) itajazwa baadaye. Juzi Dk Dk Possi alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari, akieleza kuwa alikuwa amemwandikia barua ya kujiuzulu ubunge Ndugai kutokana na Rais Magufuli kumteua kuwa Balozi.