Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.

Mabalozi walioapishwa leo ni Muhidin Ally Mboweto ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria.

Mwingine aliyeapishwa ni Wilbrod Peter Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Uteuzi wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa umeanza jana tarehe 15 Februari, 2018.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *