Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduizi, Dr Ali Mohamed Shein amewataka viongozi kuacha mtindo wa kuwakwepa wananchi na kutowajali wanapotaka taarifa za utendaji na kero zao.
Shein ameyasema hayo wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu ambazo zimeadhimishwa kwa pamoja.
Rais Shein amesema katiba iko wazi kwa wananchi kustahili kupata taarifa kutoka kwao hivyo viongozi waache mtindo wa kuwa wao si wahusika na kuna vyombo maalum vya kutoa taarifa hatua ambayo Dr Shein amepinga na kuamuru watendaji hao wabadilike na wafuata misingi ya utawala bora.