Mtangazaji maarufu nchini Uganda Robert Ogwel maarufu kama Dj Rasta Bob Mc amedai kuwa aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Zari.
Dj huyo amesema kuwa yeye ndiyo alikuwa mwanaume wa kwanza wa Zari kabla hajakimbilia kwa wanaume wenye ela na kumuacha yeye.
Dj huyo amefunguka na kudai kuwa yeye ndio alimtoa Zari kwao Jinja na kumleta jijini Kampala nchini Uganda kutokana na kuvutiwa na urembo wake.
Lakini pia amedai muda mfupi baada ya kuwa wa mjini na kupendeza ndipo Zari alivyomtosa na kuanza kutoka kimapenzi na mwanaume tajiri ambaye ni Ivan na kumwambia anaweza kuishi mwenyewe mjini na kumuacha.
Dj Rasta ambaye ni mkongwe nchini Uganda katika sekta ya burudani amekiri pamoja kuwa Zari amefanikiwa kimaisha na kutoka na wanaume matajiri lakini watambue kuwa yeye ndio alimtoa kijijini na kumfundisha kila kitu kuhusu kuishi mjini.